![Image result for mwanamitindo](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj6S_0uA29qYpGFWdnr5gB28y8emb2ViZWfdObFNd4hlwxrPJH36IWPp9CvKCwn7bPPH2y5UjEUtE7CCWY6PC5m_AAyMpgSIEsniDiO4MGWIotfgucOCxntQJyyqXjFWJUF_5KOfZg1h38/s1600/CYMERA_20140131_124322.jpg)
Sanaa ya mitindo ni sanaa inayoangaliwa kwa jicho la kipekee kutokana na umaarufu wake iliyojibebea tangu zamani za kale.Muonekano wa mwanamitindo hutokana na vitu vitatu muhimu, kitu cha kwanza ni Sura yake na
rangi yake . Sura na rangi ya ngozi yake ni kitu cha kwanza ambacho kitamsaidia mwana mitindo kuweza kuwapagawisha wafuasi wake pale tu atakapotokea jukwaani kwaajili ya kutumbuiza.
Kitu cha pili ni umbile lake au shape, kila mtu ana umbo lake lakini ili kuweza kuwa na mvuto mwanamitindo anatakiwa kuwa na umbo ambalo linamvuto kwa wengi kama umbo namba nane au kuwa na mguu wa bia na kadhalika.![Image result for mwanamitindo](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_vOE-hAG0YsXMm6Q8klC9uH3gvuynEDexnI_DRd0SGelpCylu-bAQRt88885BTf63ZutoW7UkHdtyia2aXxzzAuwCQ1EV0qWjfwLTtRvBGCafsTrwmJmvDs8SIOMAkB0jOco8LFJCukfLTq_w=s0-d)
Kitu cha tatu na chamuhimu ni mavazi, Mwanamitindo anatakiwa kuchagua mavazi ambayo yanaendana na rangi ya ngozi yake pamoja na umbo lake. Hivyo ni vitu vitatu muhimu ambavyo vinaweza kumsaidia mwanamitindo kuonekana yupo vizuri tofauti na wengine.
No comments:
Post a Comment